Tezi Dume ni Ugonjwa ambao unatambulika kama cancer inayotokea katika tezi ya mwanaume. Tezi hii inaumbo kama korosho ndogo ambayo inakazi ya kutengeneza Ute Ute zinazotumika kurutubisha na kusafirisha shahawa.
Gonjwa hili ni gonjwa ambalo kawaida huanza taratibu bila dalili zozote na kuja kujulikana baadae sana kama halikutibiwa. Tezi Dume inatabia tofauti kwa wagonjwa wake mbali mbali. Kuna wengine hutokea kidogo na haikui kabisa wagonjwa wa hivi wanaweza wasihitaji matibabu yeyote Bali Kuna wengine hukua kwa Kasi sana na kusambaa. Kwa wagonjwa wa hivi huitaji kupata matibabu mapema.
Dalili za Ugonjwa wa Tezi Dume
Kama nilivyo sema awali Ugonjwa huu unaweza usioneshe dalili zozote hapo awali bali inapokua kuwa inaweza kutambulika kwa hisia zifuatazo
- Kupata shida wakati wa kukojoa
- Mkojo kutoka wenyewe bila kuruhusu
- Mkojo kutoka ukiwa umeambatana na damu
- Shahawa kutoka zikiwa zimeambatana na damu
- Kushindwa kusimamisha zakari bila kuelewa sababu ya msingi
- Kupungua nguvu ya kurusha mkojo
- Maumivu ya mifupa
- Kupungua uzito bila kufanya jitihada yoyote
- Kukojoa mkojo mwingi kupita kiasi cha kawaida
Sababu zinazo leta Ugonjwa wa Tezi Dume
Kwa tafiti zilizo fanyika Hadi sasa hakuna maelezo kamili yanayo eleza kwamba hii ndio sababu kuu ya kupata Ugonjwa wa Tezi Dume. Hii yote ni kwasababu hutokea katika Hali ya utofauti tofauti kwa wagonjwa mbali mbali.
Ingawa kutokana na tafiti zilizo fanyika imejulikana kuwa Ugonjwa huu hutokea baada ya mabadiliko ya vinasaba (DNA) yanayotokea katika seli zilizopo kwenye Tezi yakitoa ujumbe wa kutengeneza seli nyingi katika eneo Hilo. Seli hii zinakua na kujigawanya na kuwa nyingi sizizo na tija katika eneo Hilo.
Seli hizi zikiwa nyingi zinatengeneza uvimbe katika tezi na zikizidi huvamia viungo vya jirani.
Vitu hatarishi ambavyo husababisha Tezi Dume
- Umri: umri ukishakua mkubwa kuanzia miaka 50 na kuendelea, Ugonjwa huu ni kawaida kupata kwa wanaume. Ingawa tafiti zinasema kwa sasa hata vijana kuanzia miaka 40 wapo wachache ambao washakumbana na tatizo hili
- Chimbuko la familia: kama inavyo eleweka binadamu huzaa watoto wanaofanana nao kwa vitu vingi. Hii ni kwasababu ya kurithisha sehemu ya vinasaba kwa watoto wake. Kwaio ni kawaida kama Babu au baba alishawahi kupata tatizo hili basi mtoto nae anaweza pata shida hii. Ingawa si lazima iwe ivyo
- Asili: kutokana na tafiti zilizo fanyika, imejulikana kuwa watu wenye asili ya Africa ni rahisi Sana kukumbana na tatizo hili. Ukifatilia kwa asilimia ya watu wa duniani ambao wanashida hii watu wa Africa wanaongoza kwa kupata ugonjwa huu.
- Unene uliokithiri: Tafiti zinasema watu wenye unene uliokithiri wapo kwenye hatari kubwa ya kupata Ugonjwa huu kuliko wale walio na afya njema ya kawaida. Hivyo kuzingatia afya ya mwili ni vizuri kuepukana na ugonjwa huu.
- Pombe: unywaji wa pombe kupita kiasi pia huchangia kwa kupata ugonjwa huu.
Athari za kutotibu Ugonjwa wa Tezi Dume
Endapo utaona umepata dalili tajwa hapo juu, jitahidi usifiche Wala kulea maradhi haya. Maradhi haya ni hatari sana pale endapo hautachukua hatua ya kutibiwa. Madhara ambayo unaweza pata ni
Kansa: unaweza pata kansa ambayo itasambaa katika mwili wako mzima ikianzia katika mfuko wa mkojo kwenda kwenye damu hapo husafiri katika mifumo mbali mbali ya mwili mpaka kwenye mifupa na sehemu zote za mwili. Ingawa inaweza kusambaa kiasi hiki na kumpa mgonjwa tabu sana, Ugonjwa huu unaweza tibika na kumpa mgonjwa nafuu ingaweje hawezi pona kabisa kabisa.
Kushindwa simamisha zakari: Ugonjwa huu usipo tibiwa unaweza sababisha mtu akashindwa kabisa kusimamisha zakari yake na kufurahia mapenzi na mwenza wake.
Vya kufanya ili kuepukana na Ugonjwa wa Tezi Dume
- Mlo wenye afya: Kula milo mizuri yenye afya husaidia kuepukana na ugonjwa huu. Kula chakula ambacho kitakua na mboga mboga pamoja na matunda husaidia kuepukana na ugonjwa. Nyanya ikiliwa yenyewe kama diet yako ya kila siku inasemekana kuwa ni nzuri zaidi kusaidia kupunguza hatari za ugonjwa huu
- Mazoezi: Mazoezi ya mwili mzima kama kukimbia, kucheza mpira au kuogelea husaidia kuepusha hatari za ugonjwa huu. Husaidia mwili kuzungusha damu na kutoa uchafu wote ambao huleta magonjwa mwilini kwa ujumla.
- Uzito: Zingatia usiwe na uzito mkubwa kupita kiasi. Uzito huchochea mlipuko wa ugonjwa huu kukua kwa kasi
Hivyo basi ni vyema kumuona daktari kwa ajili ya ushauri na matibabu ya Ugonjwa huu. Kawaida madaktari wa hospitalini wengi hushauri kufanya tiba kwa njia ya upasuaji. Kama utaamua kufanya tiba kwa njia hii ni vyema kutafuta daktari mzuri anae eleweka Ili akufanyie. Vinginevyo akikosea kukufanyia unaweza usipone na ukashindwa simamisha zakari yake tena katika maisha yako yanayo endelea.
Kwa ushauri ningependa nimsihii mtu yeyote ambae anaumwa Ugonjwa huu ni vyema atumie dawa ya asili ambayo inatambulika kusaidia wengi bila kufanya upasuaji wowote.
Link ya kuweza kupata dawa hii bonyeza hapa chini uweze kufika katika ukurasa huu.
You must Register or Login to post a comment